Shirika la Habari la Hawza - Kongamano kubwa la Qurani limefanyika leo hii tareh 25/5/2025 jiji Daresalamu katika viwanja vya Mnazi Mmoja huku viongozi wa dini mbalimbali na Taasisi tofauti wakihudhuria kwenye kongamano hilo, leo hii ikiwa ni kilele cha mfululizo wa mahafali hizo za Qurani, mamia ya watu waliweza kukusanyika katika viwanja hivyo na kujumuika kwa pamoja ili kusikiliza maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu.
Viongozi wa taasisi mbali mbali za kidini wakifuatilia kwa ukaribu zaidi mahafali hiyo
Tofauti na makongamano mengine yaliyowahi kufanyika siku kadhaa zilizopita, kongamano la leo liliweza kuwa ni la aina yake na la kipekee baada ya kukusanya watu wa dini tofauti wakiwemo waislamu na wasio waislamu, hii ikiwa ni ishara njema inayo onesha umoja na mshikamano katika jamii, kwani jamii inafaa kuungana na kuwa pamoja katika mambo tofauti ili kuweza kusonga mbele na kuondoa bughudha na chuki zilizo pandikizwa katika jamii hiyo kwa sababu ya dini au kitu chengine.
Mamia ya watu walioshiriki katika kongamano hilo wakifuatilia kwa ukaribu zaidi kisomo cha Qurani
Katika kongamano la leo ambalo lilikuwa na kauli mbiu isemayo "Sauti ya rehema, mkusanyiko mkubwa katika mwanga wa Qurani" liliweza kukusanya watu mashuhuri na wasimamizi wa vituo mbali mbali. Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa ni Naibu waziri (Muungano na Mazingira) Mh: Hamisi Hamza Hamisi. Vilevile Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Sheikh Jalala Hemedi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAT) sheikh Al-Hadi Mussa, Msimamizi mkuu wa chuo cha Almustafa nchini Tanzania Dkt. Ali Taqavi pamoja na msimamizi wa kituo cha Utamaduni wa wairani nchini Tanzania, wote hao ni miongoni mwa sura mashuhuri ambazo zilifanikiwa kuwasili kwenye kongamano hilo.
Wanawake wa kiislamu nao pia hawakuwa nyuma katika kuonesha ushiriki wao kwenye kongamano hilo
Maoni yako